Sunday, January 10, 2010

Shoga Azikata Nyeti za Mwanaume Aliyekataa Kumpa Mamboz


Shoga Hans O. jitu la miraba minne lenye uzito wa kilo 120, alifikishwa mahakamani mjini Dusseldorf akikabiliwa na mashtaka ya kufanya shambulio la kudhuru mwili na kumnfanyia shambulio la kijinsia mwanaume aliyekataa kufanya naye mapenzi.

Tukio hilo lilitokea septemba 2 mwaka jana wakati Hans na rafiki yake Alexander J. walipokutana kwenye mji wa Neuss, uliopo karibu na mji wa Dusseldorf. Walienda nyumbani kwa Hans na kuanza kunywa pombe kuanzia mchana mpaka usiku.

Hans alilewa sana siku hiyo na kisha kuwa mwenye hamu kubwa ya kufanya mapenzi.

Alianza kufungua vifungo vya suruali ya rafiki yake ambaye wakati huo alikuwa amelala kwenye kochi akiwa amelewa chakari.

Hans alianza kuzichezea sehemu za siri za rafiki yake kwa nia ya kumfanya apandishe mzuka ili amtimizie haja zake za kimapenzi lakini Alexander kwakuwa wakati alikuwa taabani kwa pombe alikuwa hataki kufanya chochote.

Hans alipoona juhudi zake zimegongwa mwamba, kutokana na hasira aliyakata makende ya Alexander kwa kutumia kisu na kisha kuyatupa nje kupitia dirishani.

Ingawa Alexander alipoteza damu nyingi, aliweza kujikongonya mwenyewe hadi nyumbani kwake umbali wa kilomita mbili ambapo mama yake aliita ambulansi.

Polisi baadae walifanikiwa kuyapata makende ya Alexander yakiwa yameganda kutokana na baridi nje ya nyumba ya Hans.

Alexander alitumia siku kadhaa hospitalini alikolazwa akipatiwa matibabu.


Hans alifunguliwa mashtaka mawili ya kudhuru mwili na kumfanyia shambulio la kijinsia rafiki yake. Kesi yake iliahirishwa hadi januari 13.

No comments:

Post a Comment