Tuesday, January 5, 2010

Daktari wa Nigeria Azalisha Wasichana, na Auza Watoto


Polisi nchini Nigeria wamemtia mbaroni daktari ambaye alikuwa akiwalaghai wasichana wenye umri kati ya miaka 12-17 na kuwatia mimba ili awauze watoto watakaowazaa.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa wasichana watano wenye mimba walikutwa kwenye kliniki ya daktari huyo katika mji wa Enugu uliopo mashariki mwa Nigeria.

Daktari huyo alikuwa akiwauza watoto wanaozaliwa na wasichana anaowapa ujauzito.

Polisi walisema kuwa daktari huyo amekiri kuwatia mimba wasichana zaidi ya saba na kisha kuwauza watoto waliowazaa.

Daktari huyo atapandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya kufanya mapenzi na wasichana wenye umri mdogo na kufanya biashara ya kuuza watoto.

Biashara ya kuuza watoto imeshamiri katika sehemu nyingi za nchini Nigeria ambapo watoto hununuliwa kwaajili ya kutumikishwa kwenye majumba au kutumiwa kwenye biashara ya ukahaba.

Mwaka 2008, polisi walivamia hospitali moja katika mji huo huo iliyokuwa ikijulikana kama "Shamba la Watoto" na kufanikiwa kuwaokoa wasichana saba wajawazito.

No comments:

Post a Comment