Wednesday, January 13, 2010

BECKHAM AONYESHA MICHORO YA 'YESU MPYA' MWILINI MWAKE


Michoro hiyo iko kwenye mwili wake sehemu za kifuani na mgongoni ikionyesha mchoro maarufu unaojulikana kama ‘Mtu wa Huzuni’ uliochorwa na Matthew R. Brooks, ukimwonyesha Yesu wakati akienda kuwambwa msalabani.
Mchoro huo ni wa nne katika mwili wa mwanasoka huyo ambao unaonyesha sanamu za Yesu Kristo.
Beckham tayari ana sanamu ya msalaba nyuma ya shingo yake, malaika mlinzi katikati ya mabega yake kwa nyuma na malaika mmoja kwenye bega lake la kushoto.
Malaika mlinzi yuko pale kusimamia majina ya wanae watatu ambao ni Brooklyn, Romeo and Cruz.
Beckham pia ana mchoro wa namba VII ya Kirumi katika eneo la mkono wake wa kulia ikimaanisha namba ‘saba’ ambayo aliitumia katika jezi alilokuwa akilivaa wakati akiwa na timu ya Manchester United.
Hata hivyo, mwaka 2000 alichekwa baada ya kuliandika jina la mkewe, Victoria, kwa Kihindi katika eneo la mkono wake wa kushoto, ambapo jina hilo liliandikwa likiwa na makosa kadhaa.

No comments:

Post a Comment