Basi la timu ya taifa ya Togo limeminiwa risasi wakati lilipokuwa likivuka mpaka kuingia Angola kutokea Jamhuri ya Kongo kwaajili ya mashindano ya mataifa ya Afrika yanayoanza jumapili hii nchini humo.
Dereva wa basi la timu ya taifa ya Togo aliuliwa katika shambulizi hilo ambalo jumla ya watu sita walijeruhiwa.
Makamu Rais wa shirikisho la soka la Togo Gabriel Ameyi alisema kuwa kipa wa akiba wa timu hiyo Obilale Kossi na beki wa kati Serge Akakpo ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika shambulizi hilo lililotokea leo ijumaa.
Nyota wa timu ya taifa ya Togo na Manchester City ya Uingereza, Emanuel Adebayor alikuwemo kwenye basi hilo lakini alinusurika maisha yake.
Akiongea toka nchini Togo, Ameyi alisema kuwa timu ya taifa haikutakiwa kusafiri kwa basi kwenda Angola na CAF haina taarifa kuwa Togo wametumia basi katika safari yao ya kwenda Angola.
"Tulimiminiwa risasi kama mbwa vile", alisema mchezaji wa Togo, Thomas Dossevi anayeichezea timu ya Nantes ya Ufaransa.
"Walikuwa na machine gun ... tulitumia dakika 20 chini ya viti vya basi", aliongeza Dossevi.
Dossevi aliongeza kuwa wachezaji wa Togo wanafikiria kujitoa kwenye kombe hilo.
"Tunawafikira wachezaji wenzetu ambao wamejeruhiwa kwa risasi, inasikitisha sana", aliongeza Dossevi.
Timu 16 zipo nchini Angola zikipambana kumtafuta mbabe wa Afrika ambapo Togo imepangwa kuingia uwanjani kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Ghana siku ya jumatatu.

No comments:
Post a Comment