Tuesday, January 5, 2010

JENGO REFU ZAIDI LAFUNGULIWA





Jengo hilo ambalo awali lilikuwa likijulikana kama Burj Dubai kabla ya Dubai kupewa msaada wa kifedha na Abu Dhabi baada ya kuingia kwenye madeni, lilifunguliwa kwa sherehe iliyoambatana na shoo ya fataki mbali mbali.
Jengo hilo lilibadilishwa jina na kuitwa Burj Khalifa ili kumuenzi kiongozi wa Abu Dhabi aliyeipa msaada Dubai wa dola bilioni 10.
Jengo hilo lina urefu wa mita 828 na lina ghorofa 160 ambazo ni nyingi sana kulinganisha na jengo lililokuwa likijulikana awali kama ndilo refu kuliko yote duniani la Taipei lenye ghorofa 101.
Ghorofa hilo ambalo ujenzi wake ulianza mwaka 2004, mbali ya kuwa jengo refu kuliko yote duniani ndilo pia jengo lenye lifti ndefu kuliko zote duniani.
Jengo hilo pia lina msikiti ulio juu kuliko yote duniani kwenye ghorofa ya 158 na lina bwawa kubwa la kuogelea lililo juu kuliko yote duniani kwenye ghorofa ya 76

No comments:

Post a Comment