Tuesday, January 12, 2010

Mtikila atupwa rumande


Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar imetoa amri ya kuwekwa rumande Mchungaji Christopher Mtikila ambaye anakabiliwa na kesi ya kumkashifu Rais Jakaya Kikwete kwa kukiuka amri ya mahakama na kukiuka masharti ya dhamana mara mbili

Mch. Mtikila alishtakiwa Oktoba 22 mwaka jana baada ya kumwita Rais Kikwete 'gaidi na muhuni'. Hakimu mkuu mkazi Waliarwande Lema alitoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa chama cha upinzani baada ya kutofika mahakamani asubuhi, akiwa nje kwa dhamana.

Hakimu Lema aliamuru mshtakiwa awekwe rumande hadi January 25, mwaka huu wakati kesi yake itapotajwa. Upande wa mashtaka umesema upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.

Mapema asubuhi, wakati kesi hiyo ilipotaka kuanza kusikilizwa, Mch. Mtikila alikuwa hayupo mahakamani.Wakili wa serikali, Beatrice Mpangala, aliiomba mahakama kutoa amri ya kukamatwa kwa mshatkiwa kwa kukiuka masharti ya dhamana kama ilivyokuwa Oktoba 22, mwaka jana ambapo inadaiwa haukutokea mahakamani.

Hakimu alilikubali ombi hilo na kuamuru polisi kumkamata mshtakiwa mara moja. Na Mch. Mtikila hatimaye alipowasili mahakamani hapo baadaye akajikuta anatiwa nguvuni mara tu baada ya kukanyaga viunga vya mahakama ya Kisutu.

No comments:

Post a Comment