Xie Qiuping mwanamke mwenye nywele ndefu zaidi duniani.
Mwanamke huyo ana nywele ndefu zaidi kuliko binadamu yeyote duniani, ambapo nywele hizo zina urefu wa futi 16. Nywele zake ni ndefu mno kiasi kwamba ni lazima azifunge katika chombo maalum cha kushika nywele kichwani mwake na lazima asafiri na mtu wa kumsadia kuhakikisha hazimpi matatizo.
Xie amekuwa akifuga nywele zake tangu alipokuwa mtoto mdogo. Anasema kwamba mara ya mwisho kunyoa nywele hizo ilikuwa mwaka 1973.
“Hakuna tatizo lolote. Nimezoea hali hiyo. Lakini ni lazima uvumilie kidogo unapokuwa na nywele nyingi kiasi hiki,” anasema.
Hata hivyo, pamoja na Xie kushikilia rekodi ya dunia katika urefu wa nywele, kuna mshindani wake, Cheng Shiqiong, ambaye amekuwa akizifuga nywele zake tangu mwaka 1996.
Pamoja na hivyo, Xie hana wasiwasi wowote, kwani nywele za Cheng ndiyo kwanza zimefikia nusu ya urefu wa nywele zake, yaani kiasi cha futi 8.

No comments:
Post a Comment