Sunday, January 17, 2010

MZEE WA MIAKA 100 AELEZEA SIRI YA MAZOEZI YAKE


MZEE wa miaka 100, ambaye anasemekana ndiye mtu mwenye umri mkubwa zaidi nchini Uingereza akiwa bado anaendelea kufanya mazoezi kwenye ‘gym’, ameelezea siri ya maisha yake marefu na yenye afya...
Mtu huyo, Georgina Easter, amesema siri kubwa ni kula chakula chenye lishe kamili.
"Siri yenyewe ni kuachana na vyakula ambavyo havijengi chochote mwilini,” alisema mwanamke huyo kutoka Chaddesden, Derby, Uingereza.
"Isitoshe huwa ninafanya kazi kwenye bustani yangu, napika chakula changu kila siku. Pia napenda kula maini yaliyokaangwa na vitunguu.”
Mwanamke huyo alizaliwa wakati Mfalme Edward wa Saba wa Uingereza alikuwa anashikilia taji na wakati ambapo ujenzi wa meli maarufu ya Titanic ulikuwa umefikia nusu.
Easter amewazidi kwa wastani wa miaka 30 wenzake ambao anafanya nao mazoezi ya kujiweka katika afya njema.
Freda Notley, 64, mmoja wa watu wanaofanya mazoezi na Georgina, anasema ni vigumu kuamini uwezo ambao bado anao katika mazoezi bibi huyo.
Mfanya mazoezi mwingine, Jean Bell, 71, anamsifia Georgina kwa ukakamavu wake ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli zingine nyumbani kwake.

No comments:

Post a Comment