Tuesday, January 5, 2010

Polisi Afukuzwa Kazi Kwa Kufanya Mapenzi Kanisani


Polisi mmoja nchini Ujerumani amesimamishwa kazi baada ya kuitibua misa kanisani kutokana na kelele na miguno ya kimahaba aliyokuwa akiitoa yeye na mpenzi wake wakati walipokuwa wakifanya mapenzi juu ya paa la kanisa.
Mchungaji Nikalaus Maier alikuwa akiendesha misa kanisani wakati kelele na miguno ya kimahaba ilipoanza kusikika kanisani na kuitibua misa hiyo.
Kelele hizo za kimapenzi zilikuwa zikitolewa na afisa wa polisi mwanaume aliyekuwa akifanya mapenzi na mpenzi wake kwenye mnara wa kengele za kanisa hilo.
Ilikuwa ni misa ya asubuhi ya kuukaribisha mwaka mpya katika kijiji cha Rennertshofen nchini Ujerumani wakati waumini kanisani walipoanza kuangalia juu waliposikia kelele za kimapenzi za polisi huyo na mpenzi wake.
"Mke wangu aliyekuwa amekaa nyuma kanisani aliniita aliposikia kelele za miguno ya kimahaba ambayo ilikuwa ikitibua utulivu kwenye misa", alisema afisa wa kanisa hilo Willi Black.
Mchungaji Maier aliwaita polisi wakati wapenzi hao waliposhuka chini huku wakiona aibu wakifunga vifungo vya nguo zao.
"Inanifanya nijisikie vibaya kufikiria kuwa watu wamekosa sehemu zingine za kwenda kufanyia mapenzi yao", alisema Mchungaji Maier.
Polisi huyo amesimamishwa kazi na kufunguliwa mashtaka ya kuvuruga utulivu katika sehemu ya ibada.
Taarifa zaidi zilisema kuwa polisi huyo na mpenzi wake waliamua kumalizia haja zao za kimapenzi kanisani bila kutarajia kuwa misa ya asubuhi ilikuwa inaanza muda mfupi baadae.
 






No comments:

Post a Comment