Habari za kusikitisha zilitofukia jioni hii, zinasema kuwa yule msichana aliyejulikana kwa jina la Sofia James, aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kuvimba miguu amefariki dunia. Kwa mujibu wa baba mzazi, Bw. james Mwiga, Sofia ameaga dunia majira ya saa moja jioni nyumbani kwao maeneo ya Makongo, jijini Dar es salaam. Sofia, ni msichana ambaye tatizo lake lilitolewa kwenye mtandao wa intanet miaka miwili na nusu iliyopita na kuvuta hisia za watu wengi ambao walijitokeza wakitaka kumsaidia. kulikuwa na mipango mingi ikiwemo ya kumpeleka Ulaya kutibiwa, lakini Mungu ametimiza ahadi yake kabla azma hiyo haijatimia...
MUNGU AILAZE roho ya marehemu peponi...AMIN!
No comments:
Post a Comment