Rais Kikwete pia aliwataka Watanzania kuwapuuza watu hao, ambao alieleza bayana kuwa ni wanasiasa, viongozi wa taasisi za kijamii "na hasa wa dini" kwa kuwa wataibuka na hoja hizo kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba, tena kwa nguvu kubwa zaidi.
Uongozi wa Kikwete umejikuta ukifuatiliwa kwa karibu katika siku za karibuni, na hasa rais mwenyewe ambaye ameelezewa kuwa anasita kufanya maamuzi magumu, huku CCM ikipoteza mwelekeo na kutekwa na matajiri, na ilifikia wakati wakosoaji hao walikishauri chama hicho kisimteue Kikwete kugombea urais kama atashindwa kufanya maamuzi dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.
Awali Kikwete alisema kuwa angeshangaa kama watu hao ambao ni pamoja na mawaziri wa zamani Matheo Qares na Mussa Nkangaa, wasingesema hayo na kuahidi kwenda kuandaa majibu. Lakini katika salamu zake za kuaga mwaka na kuukaribisha Mwaka Mpya, rais alidokeza kuwa kuna watu ambao hauli zao zina mwelekeo wa kuvunja amani na mshikamano na kuwataka wananchi kuendelea kuwapuuza watu hao.
Mwanasiasa mkongwe nchini, Bob Makan alisema kwamba kauli ya Kikwete imewalenga moja kwa moja wanasiasa wanaomkosoa, lakini akasema kwamba inawezekana wanafanya hivyo kwa kumsaidia na siyo kumharibia.
Alimshauri Rais Kikwete kuwa mvumilivu katika hayo na kuyatumia kama kioo cha kuangalia mapungufu ya serikali yake kwani kuwapuuza itakuwa sawa na mtu kukimbia kivuli chake.
"Kufanya hivyo ni sawa na kukimbia kivuli chake. Wanasiasa tupo kwa ajili ya kumkosoa na ndio wajibu wetu sidhani kama kuna mtu anayetaka kulivuruga taifa,"alisema Makani ambaye alistaafu uenyekiti wa Chadema.
Muasisi na mwenyekiti wa kwanza wa Chadema, Edwin Mtei alisema Rais Kikwete asingeweza kuwasema wapinzani kwa sababu wamekuwa mstari wa mbele kumueleza mapungufu ya serikali yake kwa lengo la kujenga.
Kwa mujibu wa Mtei, Rais Kikwete alilenga zaidi makundi yaliyomo ndani ya CCM kwa kuwa suala la ufisadi limewavuruga hadi wakaanza kunyoosheana vidole wenyewe kwa wenyewe.
Moja ya kauli zilizowafanya wanasiasa hao kuhisi Rais Kikwete anawashambulia ni pale aliposema: "Taifa letu limeendelea kuwa moja na watu wake wameendelea kuwa wamoja, licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale zilizotokana na harakati za vyama vya siasa na kauli za baadhi ya wanasiasa na viongozi wa kijamii na hasa wa dini.
"Wakati mwingine, matendo na kauli zao zimekuwa na mwelekeo wa kuwagawa Watanzania katika makundi yenye mifarakano na uhasama."
Katika kuonyesha kwamba matendo na kauli hizo za 'wabaya' wake zimegonga ukuta, Rais Kikwete alisema: "Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru kwa dhati Watanzania wenzangu kwa ukomavu wa kisiasa, moyo wao wa uzalendo na busara waliyotumia ya kukataa kuwa wahanga wa njama hizo ovu."
Rais Kikwete hakuishia hapo, bali aliwasifu Watanzania wengi kuwa upande wake akisema: "Mmechagua kufuata na kufanya mambo yenye maslahi kwa umoja, maendeleo na usalama wa taifa letu.
Hakika ni moyo huo na ufahamu huo ndiyo umeliweka taifa letu kuwa moja na lenye amani na utulivu tulionao tangu uhuru wa Tanganyika, mapinduzi ya Zanzibar na baadaye Muungano mpaka leo."
Hivyo akaendelea kuwasisitizia Watanzania wasirudi nyuma akiwahimiza: "Nawaomba ndugu zangu tushikilie msimamo huo hasa katika mwaka ujao wa uchaguzi ambapo haya yaliyofanywa mwaka huu yanaweza kufanywa maradufu."
Rais hakumtaja mtu yeyote kwa jina wala kutaja kauli zilizotolewa na 'waovu hao wa taifaĆ¢€™ lakini baadhi ya wachambuzi wa siasa walisema kauli zake ni sehemu ya ahadi yake aliyoitoa uwanja wa ndege aliporejea kutoka ziara ndefu iliyohusisha nchi za Jamaica, Trinidad na Tobago, Cuba na Marekani na kuwaambia waandishi wa habari atajibu shutuma dhidi ya utawala wake zilizotolewa kwenye kongamano la kutimiza miaka 10 tangu kifo cha muasisi wa taifa la Tanzania, Julius Kambarage Nyerere.
Ingawa kwenye kongamano hilo wajumbe walimlaumu rais pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushindwa kuwakamata watuhumiwa wa ufisadi, kwenye salamu zake za mwaka mpya, Rais Kikwete aliisifu taasisi hiyo kwa kufanya kazi nzuri ambapo wengi wamefikishwa mahakamani na kuahidi kwamba serikali yake itaendelea kuwa nao bega kwa bega.
"Nawapongeza sana wenzetu wa Jeshi la Polisi na Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini kwa kazi nzuri waliyoifanya. Nawaomba mwaka 2010 waongeze juhudi maradufu. Mimi naendelea kuwaahidi msaada na ushirikiano wangu na wa serikali," alisema Rais Kikwete kwenye sehemu ya salamu zake za mwaka mpya.
Kikwete anajivunia rekodi ya serikali yake kuwafikisha mahakamani mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, na katibu mkuu wa wizara, Grey Mgonja kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara, pamoja na kesi kadhaa za wizi kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).
Lakini wachambuzi wanaona kuwa kashfa ya EPA inahusisha wanasiasa na wafanyabiashara vigogo wengi ambao hadi sasa hawajafikishwa mahakamani kwa makosa ya kuchota zaidi ya Sh133 bilioni.
Pia wachambuzi wanaona kuwa rais ameshindwa kuighulikia kikamilifu kashfa ya utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa kampuni Richmond Development, kutokana na kutowawajibisha watendaji walio kwenye mamlaka yake ambao walitajwa kwenye ripoti ya kamati teule ya Bunge na maazimio 23 ya chombo hicho cha wananchi.
Suala la serikali ya Kikwete kutekeleza maazimio hayo limekuwa likipigwa danadana tangu mwaka juzi baada ya serikali kupewa miezi sita kulighulikia.
Pamoja na Kikwete kutoeleza viongozi wa dini wamefanya uovu gani, lakini mijadala iliyotikisa taifa kutokana na kuwa na udini ni suala la Waislamu kutaka serikali itekeleza ilani ya chama tawala, yaani CCM kwa kuanzisha Mahakama ya Kadhi.
Pia waraka wa Kanisa Katoliki uliotolewa kama mwongozo kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu ulisababisha mjadala mkubwa kutokana na wanasiasa kudai kuwa unaweza kuchochea tofauti za kidini.
Waraka huo ulifuatiwa na mwingine uliotolewa na Shura ya Maimamu wa Kiislamu.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment