Sunday, January 24, 2010

BREAKING NEWS - Ndege ya Ethiopia Yaanguka Baharini Ikiwa na Abiria 85


Ndege ya Ethiopia Ethiopian Airlines ikiwa imebeba abiria 85 imeripotiwa kudondoka kwenye bahari ya mediterranean muda mfupi baada ya kupaa toka uwanja wa ndege wa Beirut, Lebanon.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ndege hiyo ilitoweka kwenye rada muda mfupi baada ya kupaa kutoka Lebanon kuelekea Addis Ababa, Ethiopia.
Kwa mujibu wa tovuti ya Ethiopian Airlines ndege hiyo iliyoanguka ilikuwa ni Boeing 737.
Ilianza safari zake toka Lebanon alfajiri ya leo na ilikuwa ifike Addis Ababa masaa matano na nusu baadae.
Taarifa zaidi tutawaletea pindi zitakapopatikana.

No comments:

Post a Comment