- Kama nilivyowahi kugusia hapa, kweli kama siku zako hazijafika hazijafika tu. Mtoto wa miaka mitano amepatikana leo kule Haiti akiwa hai SIKU NANE tangu nchi hiyo ikumbwe na tetemeko kubwa la ardhi. Mama yake alifariki katika tetemeko hilo na baba yake hajulikani aliko. Haijajulikana kama mtoto huyo alikuwa na njia ya kujipatia chakula na maji katika kipindi alichokuwa chini ya kifusi. Madaktari wamesema hana mifupa iliyovunjika ingawa alikuwa ana upungufu mkubwa wa maji mwilini. Miujiza kama hii huwa inatia moyo na kuleta matumaini katika nyakati za giza kama zinazoikumba Haiti kwa sasa. Tazama video hapa na kwa habari kamili zaidi tembelea hapa.
KWINGINEKO
- Serikali ya Haiti imesema kwamba mpaka sasa maiti 72,000 wameshapatikana. Mashirika mbalimbali yanakadiria kwamba pengine watu wapatao 200,000 wameangamia katika tetemeko hilo.
- Matetemeko mengine matatu katika miaka 100 iliyopita ndiyo yaliangamiza watu wengi zaidi kuliko hili la Haiti:
1976 - China - liliua watu 225,000
2004 - lilisababisha sunami katika nchi mbalimbali za Asia na kuua watu zaidi ya 300,000.
No comments:
Post a Comment