Thursday, January 28, 2010

Wednesday, January 27, 2010

Mwanaume Mwingine Apata Mimba, Kujifungua Mwezi Ujao


Scott Moore kushoto akiwa na mumewe Thomas kulia
Scott Moore mwanaume wa nchini Marekani ambaye alizaliwa kama mwanamke anatarajia kuwa mwanaume wa pili wa nchini Marekani kupata mimba na kujifungua mtoto.

Scott anatarajia kujifungua mtoto wa kiume mwezi ujao.

Mume wa Scott ambaye naye alizaliwa mwanamke kabla ya kubadilisha jinsia na kubadilisha nyeti zake, anatarajia kuwa pembeni ya Scott wakati wa kujifungua.

Scott amejibadilisha jinsia kuwa mwanaume lakini alikubaliwa kuolewa kisheria na Thomas kwa kutumia cheti chake cha kuzaliwa ambacho kinamuonyesha kuwa yeye ni mwanamke.

Thomas yeye anahesabika mwanaume kwakuwa alibadilisha jinsia yake na kufanya operesheni ya kuuondoa uke na kuupandikiza uume.

Scott yeye bado hajafanya operesheni hiyo ya kuuondoa uke wake hivyo bado ana sehemu za siri za kike.

"Tunajua watu watatukosoa lakini sisi tuna furaha ya kupata mtoto na wala hatujisikii vibaya", alisema Scott mwenye umri wa miaka 30 ambaye alisema mtoto wao wamepanga kumpa jina la Miles.

Scott anasema kwamba alizaliwa kama mwanamke akipewa jina la Jessica na alianza kupata shauku ya kuwa mwanaume alipoanza kupevuka alipokuwa na umri wa miaka 11.

Scott aliendelea kusema kuwa wazazi wake awali walimpinga lakini baadae walimsaidia kutimiza nia yake ya kuwa mwanaume.

Alianza kumeza vidonge vya homoni za kiume alipokuwa na umri wa miaka 16 na wazazi wake walimlipia gharama za kuyaondoa matiti yake.

Scott anasema kuwa alishindwa kulipia gharama za operesheni ya kuutoa uke wake na kuupandikiza uume hivyo hadi leo bado ana sehemu za siri za kike.

Thomas kwa upande wake yeye alifanikiwa kufanya operesheni ya kuuondoa uke na kuupandikiza uume mwaka jana.

Scott alipata ujauzito baada ya kupandikizwa mbegu za kiume za mwanaume ambaye yuko karibu na familia hiyo.

Scott anasema kuwa ana mpango wa kumzaa mtoto wake kwa njia ya asili.

"Hatukutaka kuwashtua watu watakapoona mwanaume anajitokeza kuja kujifungua", alisema Scott akielezea jinsi walivyomtafuta daktari wa kumzalisha.

Scott anasema kuwa hawakumpata kirahisi daktari huyo kwani madaktari wengi walikuwa wakikwepa kuonana naye na hata kumpa matibabu.

"Tunataka kuwaonyesha watu kuwa watu waliobadilisha jinsia nao wanaweza kuanzisha familia zilizojaa upendo na furaha", alisema Thomas.


 

Mtoto Aliyezaliwa Akiwa na Miguu Minne, Mikono Minne Aanza Shule


Lakshmi Tatma alivyokuwa awali na alivyo sasa
Mtoto wa nchini India ambaye alizaliwa akiwa na miguu minne na mikono minne, ameanza shule miaka miwili baada ya kufanyiwa operesheni ya kuviondoa viungo vilivyozidi. 

KITUKO CHA LEO


Katuni Ya leo


Tuesday, January 26, 2010

Kula chakula kutoka chooni

Hizi picha ni kutoka Modern Toilet Restaurant huko Taipei, Taiwan. Viti vya kukalia ni vyoo vya kizungu. Napkins ni toilet paper, meza ni bathtubs. Hebu mtazame hizi picha. Mimi mwenyewe natamani kutapika nikiwaza kula kula chakula hapo. Wateja 100 wanaweza kuingia kwa mpigo.


 

 

 

 

 

 

 

KITUKO

Two couples were playing cards. Jeff accidentally
dropped some cards on the floor. When he bent down under the
table to pick them up, he noticed that Dave's wife,
Sandy, was not wearing any underwear! Shocked by this, Jeff
hit his head on the table and emerged red-faced.

Later when Jeffwent to the kitchen to get some refreshments, Sandy followed him and asked,
"Did you see anything under the table that you liked?" Jeff admitted, "Well, yes I did."
She said "you can have it, but it will cost you $100." After a minute or two, Jeff indicates that he is interested.

She told him that since Dave works Friday afternoons and Jeff doesn't, that Jeff should come to their house
around 2:00 PM on Friday.

Friday came and Jeff went to her house at 2:00 PM. After paying her the
$100, they went to the bedroom, had sex for a few hours and
then Jeff left.


Dave came home about 6:00 PM and asked his wife, "Did Jeff comes by
this afternoon?" Totally shocked, Sandy replied,
"Yes, he did stop by for a few minutes." Next Dave
asked, "Did Jeff give you $100?" Sandy thought,
'Oh hell, he knows!' Reluctantly she said,
"Yes, he did give me $100.."

"Good" Dave says. "Jeff came by the office this morning and
borrowed the $100 from me and said that he'd stop by our
house on his way home and pay me back.
My friend It's so good to have a friend you can
trust.

WAAFRIKA

WHY AFRICANS ARE ALWAYS TIRED

Its not laziness, here is the reason for a couple years many Africans have been blaming it on lack of sleepToo much pressure from job, poor blood, but now the real reason has been found:
We're tired because we're overworked. Here's why: The population of Africa is 800 million: 200 million are retired. That leaves 600 million.
There are 200 million in school.Which leaves 400 million to do the work.
Of this, there are 100 million employed by the government.Leaving 300 million to do the work.
50 Million are in the armed forces & related jobs.Which leaves 250 million to do the work.
Take from the total the 150 million people unemployed.
And that leaves 100 million to do the work.
At any given time there are 50 Million people in hospitals.Leaving 50 Million to do the work.
There are 20 Million people in prisons.Leaving 30 million to do the work.
1 Million are Chiefs, Kings, Queens , Presidents, Ministers,Pastors, Voodoo or Juju Masters.Leaving 29 Million to do the work.
Now, 28,999,998 Africans are out of Africa . In Europe, USA, Asia etc.That leaves just two people to do all the work.
You and me... But you're sitting on your chair, at your computer,Reading this joke instead of working............That leaves one person, only me, to do all the work

Monday, January 25, 2010

TUFANYE HESABU ZA MAISHA

A SMALL TRUTH TO MAKE LIFE 100%

If

A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z
is equal to
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26

Hard Work

H+A+R+D+W+O+R+K
8+1+18+4+23+15+18+11 = 98%

Knowledge
K+N+O+W+L+E+D+G+E
11+14+15+23+12+5+4+7+5 = 96%

Love
L+O+V+E
12+15+22+5 = 54%

Luck
L+U+C+K
12+21+3+11 = 47%
( don't most of us think this is the most important ??? )
Then what makes 100% ?
Is it Money ? ... NO ! ! !

M+O+N+E+Y
13+15+14+5+25 = 72%
Leadership ? ... NO ! ! !

L+E+A+D+E+R+S+H+I+P
12+5+1+4+5+18+19+9+16 = 89%

Every problem has a solution, only if we perhaps change our attitude.
To go to the top,
to that 100% ,
what we really need to go further... a bit more...

ATTITUDE
A+T+T+I+T+U+D+E 1+20+20+9+20+21+4+5 = 100%


I
t is OUR ATTITUDE towards Life and Work that makes OUR Life 100% ! ! !
ATTITUDE IS EVERYTHING
Change Your Attitude …
And You Change Your Life ! ! !
Now that you know the answer…

THE LEAST YOU CAN DO IS TO SHARE THIS MESSAGE WITH THOSE YOU CARE

WHAT WILL YOU DO ABOUT IT ?

Somo La Leo


Check maholi yetu yakujidai kitaa na kucheck boli


Sunday, January 24, 2010

Ronaldo Amvunja Pua Mchezaji Mwenzake


Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo aliifungia timu yake magoli mawili ya ushindi dhidi ya timu ya Malaga lakini alitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu baada ya kumvunja pua mchezaji wa Malaga.

Mapigano ya Waislamu na Wakristo Nigeria, Maiti 150 Zaopolewa Visimani




Maiti 150 zimeopolewa toka kwenye visima vya maji kufuatia mapambano yanayoendelea nchini Nigeria kati ya waislamu na Wakristo.

BREAKING NEWS - Ndege ya Ethiopia Yaanguka Baharini Ikiwa na Abiria 85


Ndege ya Ethiopia Ethiopian Airlines ikiwa imebeba abiria 85 imeripotiwa kudondoka kwenye bahari ya mediterranean muda mfupi baada ya kupaa toka uwanja wa ndege wa Beirut, Lebanon.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ndege hiyo ilitoweka kwenye rada muda mfupi baada ya kupaa kutoka Lebanon kuelekea Addis Ababa, Ethiopia.
Kwa mujibu wa tovuti ya Ethiopian Airlines ndege hiyo iliyoanguka ilikuwa ni Boeing 737.
Ilianza safari zake toka Lebanon alfajiri ya leo na ilikuwa ifike Addis Ababa masaa matano na nusu baadae.
Taarifa zaidi tutawaletea pindi zitakapopatikana.

Friday, January 22, 2010

Katuni yetu ya Leo


Taswira ya mwaka toka haiti


baada ya siku 10 kupita toka tetemeko la ardhi liikumbe haiti, dogo anaibuliwa kutoka kwenye kifusi na badala ya kutoka analia ananyanyua mikono juu na kushangilia kwa kusevu. kila mtu anamshangilia...hakika ni taswira itayopata sifa zote mwaka huu

Thursday, January 21, 2010

KALI YA MWAKA - Mtangazaji wa Italia Amfedhehesha David Beckham


Mtangazaji mwanamke wa televisheni moja ya nchini Italia alimuacha nyota wa soka wa Uingereza David Beckham akiuma meno kwa hasira na fedheha baada ya mtangazaji huyo kuyakamata makende yake akiwa na nia ya kujua ukubwa wake.
Huku akipiga kelele kwa kitaliano "E piccolo, Beckham" ("Beckham kumbe ni Mdogo") mtangazaji huyo alizolewa msobe msobe na walinzi wa David Beckham baada ya kuyakamata makende yake.
Mtangazaji huyo wa televisheni moja ya nchini Italia aliyejulikana kama Elena Di Cioccio alikuwa na nia ya kujua ukweli kama mali za siri za David Beckham ni kubwa kama zinavyoonekana kwenye tangazo la chupi za Armani ambalo David Beckham alishiriki.
"Nilitaka kujua ukubwa wa makende yake", alisema Elena.
Beckham alikuwa akiongea na waandishi wa habari nje ya hoteli moja mjini Milan wakati tukio hilo lilipotokea na kumwacha Beckham akiwa hajui la kufanya akibaki anamwangalia mtangazaji huyo kabla ya walinzi wake kumuondosha.
Mtangazaji huyo alipanga tukio hilo mapema na kuongozana na timu yake ya wapiga picha hadi kwenye eneo ambalo David Beckham alikuwa akiongea na waandishi wa habari.
Huku akiwa amevaa gloves za njano, mtangazaji huyo alijipenyeza na kumsogelea kwa karibu Beckham kabla ya kuzikamata nyeti zake na kuanza kupiga kelele za "Beckham kumbe mdogo".
Beckham alishiriki kwenye matangazo ya nguo za ndani za mwanamitindo maarufu duniani Giorgio Armani. Katika picha za tangazo hilo Beckham anaonekana akiwa ameshehena mzigo kwenye sehemu zake nyeti ambao mkewe Victoria Beckham aliubatiza jina la "Golden Balls".
Hivi karibuni Cristiano Ronaldo alichukua nafasi ya Beckham katika matangazo hayo ya viwalo vya ndani vya Armani.
 

NANI ALISEMA ETI WAAFRIKA SI WADADISI?


Unaiona hii pool table? Si ajabu ukakuta hata wana sheria zao wenyewe zinazoendana na mazingira yao...

MNAKARIBISHWA KANISANI, LAKINI MCHUNGE NDIMI ZENU KWANI.....


MIUJIZA KUTOKA HAITI: MTOTO WA MIAKA MITANO AKUTWA AKIWA HAI BAADA YA SIKU NANE


  • Kama nilivyowahi kugusia hapa, kweli kama siku zako hazijafika hazijafika tu. Mtoto wa miaka mitano amepatikana leo kule Haiti akiwa hai SIKU NANE tangu nchi hiyo ikumbwe na tetemeko kubwa la ardhi. Mama yake alifariki katika tetemeko hilo na baba yake hajulikani aliko. Haijajulikana kama mtoto huyo alikuwa na njia ya kujipatia chakula na maji katika kipindi alichokuwa chini ya kifusi. Madaktari wamesema hana mifupa iliyovunjika ingawa alikuwa ana upungufu mkubwa wa maji mwilini. Miujiza kama hii huwa inatia moyo na kuleta matumaini katika nyakati za giza kama zinazoikumba Haiti kwa sasa. Tazama video hapa na kwa habari kamili zaidi tembelea hapa.
KWINGINEKO
  • Serikali ya Haiti imesema kwamba mpaka sasa maiti 72,000 wameshapatikana. Mashirika mbalimbali yanakadiria kwamba pengine watu wapatao 200,000 wameangamia katika tetemeko hilo.
  • Matetemeko mengine matatu katika miaka 100 iliyopita ndiyo yaliangamiza watu wengi zaidi kuliko hili la Haiti:
1920 - China - liliua watu 200,000 au zaidi
1976 - China - liliua watu 225,000
2004 - lilisababisha sunami katika nchi mbalimbali za Asia na kuua watu zaidi ya 300,000.

WIVU WA OBAMA


Obama ana wivu kama mswahili yaani alipogundua Berlusconi wa Italy kiwembe akawa anazuia mkewe asikumbatiwe!!! Jama hajazoea salamu za mikono.

JK ANG'AKA


RAIS Jakaya Kikwete jana aligeuka mbogo na kumtimua Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro, Kayange Jacob ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kubaini kuwa wasaidizi wake wamemdanganya.
Mbali na kumtimua mkurugenzi huyo, Rais Kikwete ambaye alitakiwa kukabidhi magari ya wagonjwa kwa halmashauri za wilaya za Mbozi na Longido, aliondoka katika hafla hiyo kwa hasira bila kugawa magari hayo.
Ingawa baadaye jioni ya jana taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ilieleza kuwa Rais alimkabidhi Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Mbozi, Levison Jeremiah Chilewa kwa ajili ya wakazi wa eneo la Kamsamba, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya, gari la wagonjwa ili kupunguza shida ya usafiri wa wagonjwa katika eneo hilo.
Rais Kikwete alifika katika viwanja vya Ikulu saa 7:30 kwa ajili ya kukabidhi magari hayo ya wagonjwa, lakini, kabla ya kuanza kazi hiyo, alimhoji mmoja wa wakurugenzi ambao wilaya zao zilipaswa kupata mgawo huo.
“Wewe bwana unatoka wapi? alihoji Rais Kikwete na mkurugenzi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kayange Jacob alijibu ametoka wilaya ya Ngorongoro.
“Unasema unatoka Ngorongoro?" aliendelea kuhoji Rais Kikwete. "Hapa umefikaje, umekuja kufanya nini na nani kakualika? Aliendelea kuhoji huku akiwageukia wasaidizi wake akiwemo Katibu wa Rais Ikulu.
"Huyu amekuja kufanya nini hapa? Nani kamwalika", alisema Rais Kikwete ambaye sura yake ilionekana wazi kukasirika na kulazimia kuvua miwani.
“Hatuwezi kukupa gari hii. Hii ni kashfa kubwa, nakumbuka vizuri msaada huu niliahidi kwa wananchi wa wilaya ya Longido wakati nilipofanya ziara kijiji cha Engalinaibo kipindi cha ukame ambapo nilifika Kituo cha Afya wakazi wa Engalinaibo wakaniambia hawana gari la wagonjwa na nikawaahidi nitawaletea:
“Nakumbuka nilipofanya ziara wananchi wale waliniambia wanayo dispensary (Zahanati ) lakini, hawana gari la wagonjwa na sio nyinyi! Hatukupi bwana, sio lako hatukupi."
"Hatuwezi kukupa gari, watafuteni wanaopaswa kupewa gari hili, hii ni kashfa kubwa, document zote zimeandikwa kwa kijiji cha Engalinaibo iweje tuwape watu wa Ngorongoro?" alihoji.
“Waombeni radhi hawa mabwana (waandishi) mliowaalika kwa ajili ya kufanya coverage hii (kuandika habari hii) kwa kuwasumbua, siwezi kutoa gari hapa waende tu, ”alisisitiza Kikwete na kuondoka eneo la tukio kwa hasira bila kukabidhi magari hayo.

Wednesday, January 20, 2010

Mwanasiasa Zambia Atishia Kumbaka ´Mande´ Mpinzani wa Rais


Kiongozi wa umoja wa vijana wa chama tawala nchini Zambia ametishia kuwa vijana wa chama hicho watambaka ´mande´ mwanasiasa mwanamke anayeonyesha upinzani wa sera za rais wa Zambia.

Msichana wa Miaka 13 Kuchapwa Bakora 90 Kwa Kumshambulia Mwalimu Wake


Msichana mwenye umri wa miaka 13 wa nchini Saudi Arabia amehukumiwa kuchapwa bakora 90 kwa kosa la kumshambulia mwalimu wake aliyemnyang´anya simu yake kwa kuwa ina kamera.

Msichana wa India Anayevuja Damu Mara 50 Kwa Siku


Msichana Twinkle Dwivedi mwenye umri wa miaka 14 wa nchini India anasumbuliwa na ugonjwa ambao umewafanya madaktari wakune vichwa sana bila majibu. Mwili wa Twinkle huvuja damu mara 50 kwa siku kupitia kwenye macho yake, pua, masikio na kwenye nyayo zake.

Mtoto wa miaka miwili, mvuta sigara mdogo zaidi duniani


Mtoto huyo huvuta paketi moja ya sigara kila siku na hushikwa na hamaki iwapo hapewi kiburudisho chake hicho.
Mtoto huyo, Tong Liangliang, alifundishwa jinsi ya kuwasha sigara na baba yake ambaye aliamini kwamba uvutaji ungempunguzia maumivu ya ugonjwa wa ngiri (hernia).
‘Baba-mtu hakujua jinsi tabia hiyo ingekolea kwa kitoto chake hicho hadi pale alipong’amua kwamba idadi ya sigara kilichokuwa kinavuta kila siku ilikuwa imeongezeka,” kilitangaza kituo cha China Radio International.
Tong alianza kuvuta sigara yake ya kwanza akiwa na umri wa miezi 18 katika jitihada za kupunguza maumivu ya ngiri yaliyokuwa yanamsumbua. Hili lilifanyika kwa kutambua kwamba mtoto huyo alikuwa ni mdogo mno kiasi cha kutoweza kufanyiwa opasuaji.
Hata hivyo, hii ni “rekodi ya dunia isiyokuwa rasmi” kwa vile kuingizwa kwake katika Kitabu cha Rekodi za Guiness (Guinness Book of Records) kama mvutaji mdogo zaidi wa sigara duniani, kutakataliwa kwa madai kwamba kitendo hicho kilichochea tabia yenye madhara kwa watoto.

Tuesday, January 19, 2010

Katuni yetu ya Leo


UMEIONA HII!? YAWAHUDUMU KUWAPA JOTO WATEJA WAO?


Wapasha joto vitanda, Jacqui Barry na Nick Woods (pichani) walitoa huduma hiyo kwa Laurence Lancashire (katikati) kwenye hoteli ya Holiday Inn Kingston-South huko Surbiton, Surrey wakati wa baridi kali hivi majuzi.

HOLIDAY Inn, kampuni lenye mahoteli zaidi ya 4,000 duniani, litaanza kutoa huduma ya bure ya dakika tano ambapo binadamu watatumika kupasha joto vitanda katika hoteli yake ya London Kinsington kwa siku zote za wiki...

MWANAMKE MWENYE NYWELE NDEFU ZAIDI DUNIANI


Xie Qiuping mwanamke mwenye nywele ndefu zaidi duniani.
Mwanamke huyo ana nywele ndefu zaidi kuliko binadamu yeyote duniani, ambapo nywele hizo zina urefu wa futi 16. Nywele zake ni ndefu mno kiasi kwamba ni lazima azifunge katika chombo maalum cha kushika nywele kichwani mwake na lazima asafiri na mtu wa kumsadia kuhakikisha hazimpi matatizo.
Xie amekuwa akifuga nywele zake tangu alipokuwa mtoto mdogo. Anasema kwamba mara ya mwisho kunyoa nywele hizo ilikuwa mwaka 1973.
“Hakuna tatizo lolote. Nimezoea hali hiyo. Lakini ni lazima uvumilie kidogo unapokuwa na nywele nyingi kiasi hiki,” anasema.
Hata hivyo, pamoja na Xie kushikilia rekodi ya dunia katika urefu wa nywele, kuna mshindani wake, Cheng Shiqiong, ambaye amekuwa akizifuga nywele zake tangu mwaka 1996.
Pamoja na hivyo, Xie hana wasiwasi wowote, kwani nywele za Cheng ndiyo kwanza zimefikia nusu ya urefu wa nywele zake, yaani kiasi cha futi 8.
 

Walinzi wa Kivita Kuzilinda Timu Zitakazoshiriki Kombe la Dunia


Baada ya basi la wachezaji wa Togo kushambuliwa kwa risasi nchini Angola wakati wakiwasili kwaajili ya kombe la mataifa ya Afrika, timu zitakazoshiriki kombe la dunia nchini Afrika Kusini baadae mwaka huu zinakusudia kukodisha walinzi wa kivita toka nchini Iraq na Afghanistan.

Mama Afanya Mapenzi Mara 200 na Mtoto wa Miaka 12


Mama mmoja nchini Uingereza alifanya mapenzi mara 200 na mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 na alikuwa akiweka alama kwenye daftari lake kila alipomaliza kufanya naye mapenzi.

Vibonge Kuanza Kulipishwa Nauli za Watu Wawili Kwenye Ndege


Mashirika ya ndege ya KLM na Air France yataanza kuwalipisha nauli za watu wawili, watu wanene ambao wanashindwa kujibana kwenye siti moja.

Monday, January 18, 2010

HUPATI CHOO MARA KWA MARA? SOMA HAPA!


Ukosefu wa choo ni tatizo sugu la kiafya linalowakabili watu wengi, wengine bila kujua kama ni tatizo, huchukulia kuwa ni hali ya kawaida. Ukweli ni kwamba ukosefu wa choo ndiyo chanzo cha maradhi mengi, yakiwemo magonjwa ya moyo.

Ili mtu apate choo, angalau mara moja kwa siku, anahitaji kula vyakula vinavyosagika kirahisi tumboni. Vyakula hivyo ni vile ambavyo vina kiasi kikubwa cha kamba lishe na kiasi kidogo sana cha mafuta. Aina hii ya vyakula huwa muhimu sana, hasa kwa wale watu wenye matatizo ya kuumwa tumbo mara kwa mara.

Kwa kujijua hali hiyo na kuamua kula vyakula vyepesi, mgonjwa anaweza kupata ahueni haraka zaidi kuliko mtu anayekula vyakula vigumu. Si ajabu kuona wazee wanashauriwa kula aina hii ya vyakula kwa sababu mfumo wao wa usagaji chakula tumboni huwa hauna nguvu ya kusagaa vyakula vigumu.
VYAKULA RAHISI KUSAGIKA TUMBONI
Unapoenda sokoni au dukani kununua mahitajai yako ya chakula, ni muhimu sana kuzingatia ubora wa chakula ikiwa na pamoja na kuwa na sifa ya kusagika kirahisi tumboni. Kuna baadhi ya watu wanadai kwamba kutokana na hali halisi ilivyo, hakuna vyakula vingi vya kuchagua ili kukidhi haja hiyo, madai ambayo siyo kweli, kwani Mungu katujaalia vyakula bora vya kila aina:
MBOGA ZA MAJANI NA MATUNDA
Mboga za majani, hasa zile za rangi ya kijani kama kabichi, ni rahisi sana kusagika tumboni. Mboga za majani zina kiwango kikubwa cha vitamini na madini na husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni. Halikadhalika matunda ya aina mbalimbali, kama vile mapapai na embe, ni muhimu kuliwa. Mbali ya vyakula hivi kusaidia usagaji wa chakula, lakini pia ni lishe muhimu kwa kupunguza uzito.

WALI
Katika mlo wako wa kila siku, ambao unazingatia lishe bora, inashauriwa sana kujumuisha wali, tena kwa wingi. Mchele una virutubisho ambavyo husaidia mchakato wa usagaji chakula tumboni, hivyo kumuwezesha mlaji kupata choo kirahisi.

NYAMA YA KUKU
Nyama ya kuku nayo imo kwenye orodha ya vyakula vinavyosagika kirahisi tumboni. Lakini ni muhimu sana kujua ni aina gani ya nyama ya kuku unayotakiwa kula. Unapokula nyama ya kuku, hakikisha unaondoa ngozi na kula nyama pekee bila ngozi, ambayo huwa na mafuta mabaya yanayodhoofisha mfumo wa usagaji chakula tumboni.
NDIZI MBIVU
Miongoni mwa sababu kubwa zinazolifanya tunda hili liendelee kuwa maarufu duniani ni uwezo wake wa kurahisisha usagaji chakula tumboni. Utafiti wa kisayansi umethibitisha kuwa ‘vimeng’enyo’ vilivyomo kwenye ndizi huimarisha mfumo wa usagaji chakula tumboni. Hata watoto wachanga na wadogo wenye matatizo ya kuchafuka tumbo wanaweza kupewa ndizi mbivu kama tiba mbadala.

MAKATE WA TOSTI
Inaelezwa kuwa mkate wa tosti unasagika kirahisi sana tumboni kuliko kula mkate mkavu, hivyo unashauriwa kutosti mkate wako na kula kama kifungua kinywa na bila shaka hutasumbuliwa na ukosefu wa choo kama mtu anayekula mkate mkavu.

KIASI CHA MLO
Kiasi unachokula kwa siku ni miongoni mwa vitu vya kuzingatia linapokuja suala la usagaji chakula tumboni. Watu wengi hufanya makosa kwa kula na kushiba kupita kiasi na kujikuta wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa choo licha ya kula vyakula tulivyovitaja awali. Unashauriwa kula kiasi kidogo cha mlo kila baada ya muda, hata mara tano kwa siku, badala ya kula milo miwili mikubwa sana kwa siku.
MWISHO, jenga mazoe ya kula vyakula laini vinavyosagika kirahisi tumboni na epuka vyakula vinavyochangia ukosefgu wa choo. Vyakula vinachangaia kudhoofisha mfumo wa usagaji tumboni ni pamoja na vyakula vya kukaanga kwa mafuta mengi kama vile chips, vitumbua, mandazi, n.k. na ukosefu wa maji kunakosababishwa na mtu mwenywe kwa kutokunywa maji mengi kila siku.

Hali ilivyo Nchini Haiti ni Mfano wa Jahanamu

Maiti zikiwa zimezagaa kila kona ya mitaa ya mji mkuu wa Haiti

Hali iliyopo nchini Haiti baada ya tetemeko kubwa la ardhi inatisha sana hakuna tena utawala wa sheria mwenye nguvu anamuonea mnyonge ili apate chochote cha kukaganga njaa, maiti zimezagaa kila kona kiasi cha kwamba zinatumiwa kama vizuizi vya barabarani.
Jinsi siku zinavyozidi kwenda mbele mamia ya watu wanazidi kufariki kutokana na njaa na maradhi mbali mbali huku maelfu ya watu wakiwa wamezikwa hai chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchini Haiti.
Tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 limeuharibu kwa asilimia 90 mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.
Majengo mengi sana likiwemo jengo la ikulu na jengo la Umoja wa mataifa nchini Haiti yameporomoka na kuwafukia maelfu ya watu.
Hadi sasa jumla ya watu 50,000 wameishatibitishwa kufariki na idadi kamili ya watu waliofariki inakisiwa kuwa zaidi ya watu 200,000.
Maiti zimezagaa kila kona kiasi cha kwamba watu ambao walishindwa kupata msaada ulioletwa na mataifa ya nje waliamua kuzikusanya maiti na kuzijaza barabarani kuonyesha hasira zao.
Wezi nao wameongezeka kila kona, mwizi mmoja ambaye alikamatwa akimuibia mmoja wa wahanga wa tetemeko hilo la ardhi aliuliwa na kisha maiti yake kuburuzwa barabarani kabla ya kuchomwa moto.
Kwa hali iliyopo sasa nchini Haiti, kila mtu anajiangalia mwenyewe. Watu wenye nguvu wamekuwa wakitumia silaha zao kama vile visu na silaha nyinginezo kuwatishia watu wengine ili waweze kuwanyang'anya mali zao.
Misaada toka mataifa mbali mbali duniani imesaidia kuokoa maisha ya baadhi ya watu lakini bado haitoshi na haijawafikia watu wengi kutokana na kuharibika kwa njia zote za mawasiliano.
Hospitali zote zimefurika wagonjwa na maiti zimezagaa pia kila kona kiasi cha kwamba zimekuwa zikikusanywa na kulundikwa pamoja maiti za wanyama vile.
 

Mchezaji Mweusi wa Marekani Abadili Rangi ya Ngozi Yake


Mmarekani mweusi Sammy Sosa ambaye aliwika sana enzi zake kwenye mchezo wa Baseball amebadili rangi ya ngozi yake kutoka nyeusi kuwa nyeupe kama mzungu.
Mchezaji maarufu wa zamani wa Baseball, Sammy Sosa mwenye umri wa miaka 41 amejibadilisha rangi ya ngozi yake kuwa mweupe kama mzungu kwa kutumia krimu za kujichubua.
Sosa alianza kujichubua kuanzia mwaka 2007 na wiki iliyopita alionekana kwenye tuzo za Latin Grammy jijini Las Vegas akiwa hana tena rangi yake nyeusi ya kuonyesha asili yake ya Afrika.
Sosa alionekana mweupe kama mzungu na kwa watu ambao hawamfahamu ni vigumu kuamini alikuwa mweusi 'tii' zamani.
Sosa amesema kuwa nia yake kubadili rangi ya ngozi yake ni kutokana na mapenzi yake mwenyewe na si kumuiga marehemu mfalme wa muziki wa Pop, Michael Jackson.
Sosa amekiri pia kubadilika kwa rangi hakutokani na maradhi yoyote ya ngozi bali ni kutokana na krimu anayoitumia ambayo alisema ataipigia kampeni za kibiashara.
Hivi karibuni idadi ya watu weusi wanaojichubua nchini Marekani ili wakubalike katika soko la wazungu imezidi kuongezeka na wataalamu wa ngozi wanaonya kuwa matumizi ya krimu kujichubua ni hatari kwa afya.
Magonjwa mengi ya ngozi kama vile kansa ya ngozi yamekuwa yakihusishwa na madawa na krimu za kujichubua.
 

Sunday, January 17, 2010

WCLEF ATOA MSAADA MKUBWA KWA WAHAITI WENZAKE


Mwanamuziki huyu, ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya Haiti, ameonesha mfano wa kuiga kwa kuanzisha kampeni kwa ajili ya kuwasaidia Wahaiti wenzake walioathirika wa tetemeko la ardhi...hadi sasa ameshachangisha zaidi ya shilingi za Kitanzania Bilioni 1!

MBWA MZEE ZAIDI DUNIANI AFARIKI


* Mmiliki wake amlilia kama mwanaye
MMILIKI wa mbwa mzee zaidi duniani ambaye alikufa kutokana na kansa ya tumbo ametoa heshima zote kwa mnyama huyo ambaye alikuwa kipenzi chake...
Mbwa huyo aliyekuwa akiitwa Otto, na aliyekuwa na umri wa miaka 20 alikufa siku ya ijumaa, mwili wake utachomwa na majivu yake kuzikwa.
Mmiliki wa mbwa huyo, mwanamke Lynn Jones, 54, kutoka Shrewsbury, Shropshire, Uingereza, alisema: "Nililia siku nzima tangu asubuhi. Kwangu hili ni balaa kubwa.
"Alikufa saa nne na dakika kumi asubuhi siku ya ijumaa. Hapa nilipo naona kama nimepoteza mkono wangu wa kulia. Kwangu alikuwa kama mtoto wangu wa kiume.
“Ninafurahi tu kwamba hateseki tena na maumivu, lakini nilitaka kuwa naye milele.”
Bi Jones na mumewe Peter, 68, walimpeleka Otto kwenye kituo cha tiba za wanyama ili akauawe baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi.
"Tuligundua alikuwa na uvimbe mkubwa tumboni. Hakuweza kukaa au kulala kwa raha. Hivyo tulimpeleka kwa madaktari wa wanyama akauawe ili kuyamaliza mateso yake,” alisema Jones.
Otto, ambaye angekuwa na umri wa miaka 21 tarehe 14 Februari mwaka huu, ndiye mbwa mzee zaidi aliyetajwa katika kitabu cha Guinness Book of Records mwezi Oktoba mwaka jana.


MZEE WA MIAKA 100 AELEZEA SIRI YA MAZOEZI YAKE


MZEE wa miaka 100, ambaye anasemekana ndiye mtu mwenye umri mkubwa zaidi nchini Uingereza akiwa bado anaendelea kufanya mazoezi kwenye ‘gym’, ameelezea siri ya maisha yake marefu na yenye afya...
Mtu huyo, Georgina Easter, amesema siri kubwa ni kula chakula chenye lishe kamili.
"Siri yenyewe ni kuachana na vyakula ambavyo havijengi chochote mwilini,” alisema mwanamke huyo kutoka Chaddesden, Derby, Uingereza.
"Isitoshe huwa ninafanya kazi kwenye bustani yangu, napika chakula changu kila siku. Pia napenda kula maini yaliyokaangwa na vitunguu.”
Mwanamke huyo alizaliwa wakati Mfalme Edward wa Saba wa Uingereza alikuwa anashikilia taji na wakati ambapo ujenzi wa meli maarufu ya Titanic ulikuwa umefikia nusu.
Easter amewazidi kwa wastani wa miaka 30 wenzake ambao anafanya nao mazoezi ya kujiweka katika afya njema.
Freda Notley, 64, mmoja wa watu wanaofanya mazoezi na Georgina, anasema ni vigumu kuamini uwezo ambao bado anao katika mazoezi bibi huyo.
Mfanya mazoezi mwingine, Jean Bell, 71, anamsifia Georgina kwa ukakamavu wake ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli zingine nyumbani kwake.

SENEGAL YAWAKARIBISHA WATU WA HAITI


Rais Abdoulaye Wade alisema watu wa Haiti ni wana wa Afrika kwani Haiti ilianzishwa na watumwa waliochukuliwa kutoka Afrika na baadhi wakiaminika kutoka Senegal.
“Rais anatoa fursa hiyo kwa watu wa Haiti watakaokubali kwa hiari yao kurejea katika shina lao,” alisema msemaji wa rais, Mamadou Bemba Ndiaye.
Jumanne iliyopita makumi ya maelfu ya watu waliuawa na wengine kukosa makazi baada ya nchi hiyo kukumbwa na tetemeko la ardhi.
Majengo yameteketea na utoaji wa misaada unakwenda taratibu mno huku watu wakiondoka katika mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince, ambao umeharibiwa vibaya.
“Senegal iko tayari kuwapatia ardhi na hata maeneo makubwa zaidi. Hii itategemea ni watu wangapi wa Haiti watakaoamua kuja,” alisema Ndiaye.

Friday, January 15, 2010

UBUNIFU "HUMMER HT7 MADE IN MUSOMA"


Support your local businessman, this ride is already at the taxi rank.

 

sofa  

 

sideways

 

back side

 

Speak of innovation in Africa

Mwanaume mfupi na mrefu kuliko wote duniani wakutana


Mwanaume mfupi kuliko wote dunia, He Pingping (kushoto) raia wa China na Sultan Kosen wa Uturuki (kulia) ambaye anadaiwa kuwa mrefu kuliko wote dunia, walikutana Januari 14 mwaka huu na kupiga picha ya pamoja na kuchagua pozi poa kama wanavyoonekana pichani huko mjini Istanbul nchini Uturuki.
He ana urefu wa sentimita 73 (futi 2 na inchi 5) na Kosen ana urefu wa sentimita 246.5 (futi 8 na inchi 1) na He ameorodheshwa kwenye rekodi ya dunia ya Guiness kuwa ni mwanaume mfupi kuliko wote duniani na huku Kosen akiwa na rekodi ya kuwa mrefu zaidi duniani.