Monday, March 29, 2010

WAZIRI AFUNGA NDOA YA KISHOGA

Ndoa hiyo ilikuwa ya kwanza kufanyika katika viwanja vya jengo hilo la Bunge baada ya Spika John Bercow kupata leseni husika kutoka Halmashauri ya Jiji ya Westminster.
Katika taarifa iliyotolewa baadaye, wanandoa hao walisema walikuwa na “furaha kubwa” kwa Bw. Bercow na kiongozi wa Bunge la Makabwela, Harriet Harman kwa “kufanikisha siku hiyo maalum”.
"Hatukufikri siku hii ingefika, hatukuhangaika kuhusu keki, maua na pete,” walisema na kuongeza: “Ni ajabu hivi sasa mambo yamebadilika katika muda mfupi. Zamani mashoga walikuwa hawawezi kuoana bila kufikia umri fulani, walikuwa wanabaguliwa mpaka jeshini, hawakuruhusiwa kuoana au kupewa watoto wa kuasili.”
Walilisifia bunge kwa kufanikisha jambo hilo na kwamba kila mtu nchini Uingereza angepata fursa hiyo ambayo ilikuwa adimu.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, mwaka jana aliruhusu madai ya watu wa jinsia moja kuoana.
Hivyo ndoa zinaweza kufanyika katika viwanja vya Bunge, lakini si katika kanisa la sehemu hiyo ambalo halikubaliani na ndoa za watu wa jinsia moja.

No comments:

Post a Comment