Thursday, March 4, 2010

Kondomu Ndogo Kwaajili ya Watoto Zaingia Madukani

 
Kondomu zenye ukubwa wa wastani zinadaiwa kuwa haziwatoshi ipasavyo vijana wenye umri mdogo

Kampuni kubwa ya kutengeneza kondomu ya Uswizi imetengeneza kondomu ndogo sana kwaajili ya watoto kuanzia umri wa miaka 12 kutokana na kile kinachosemwa kuwa watoto wa siku hizi wanaanza kufanya ngono mapema.
Kondomu hizo zilizopewa jina la "Hotshot" ni maalumu kwa vijana wa kiume wenye umri mdogo kuanzia umri wa miaka 12 hadi miaka 14.

Kondomu hizo zilitengenezwa kufuatia hatua ya makundi ya uzazi wa mpango kusema kuwa vijana wenye umri mdogo hawapati kinga inayotakikana wakati wa kujamiiana.

Ilidaiwa kuwa vijana wa siku hizi wanaanza ngono mapema na hawatumii kinga na wala hawajui jinsi ya kujikinga na magonjwa yanayotokana na ufanyaji wa ngono zisizo salama.

Kondomu hizo zimeingia madukani nchini Uswizi na kuzua maoni tofauti toka kwa wazazi nchini Uswizi.

Taarifa ya utafiti uliofanyika kabla ya kutengenezwa kwa kondomu hizo ilionyesha kuhitajika kwa elimu ya mapema kwa vijana jinsi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa pamoja na mimba zisizohitajika.

Msemaji wa kampuni ya Lamprecht AG iliyotengeneza kondomu hizo, alisema kuwa watakapoanza kuuza kondomu hizo nje ya nchi, Uingereza itapewa nafasi kubwa kutokana na idadi kubwa ya mimba za wasichana wenye umri mdogo.

Katika nchi za ulaya Uingereza inaoongoza kwa idadi kubwa ya wasichana wanaopata ujauzito kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
  

No comments:

Post a Comment