Håvve Fjell, Mtu asiyesikia maumivu akiwa katika kazi zake.Håvve Fjell hujaribu kuonyesha kwamba huwa hasikii maumivu. Maonyesho anayoyafanya jamaa huyo wa Norway, hakika yanapagawisha kiasi cha kuonekana kwamba si jambo la kweli kwa mtu mwenye hisia za asili...
Baada ya kuanzisha sanaa hiyo aliyoiita “Pain Solution” mwaka 1993, Fjell alipata fursa ya kushirikiana na watu wengi walioipenda, na leo hii watu wengi zaidi hupenda kusoma kitabu chake kiitwacho "Kvintett," ambacho kinaonyesha mfululizo wa maonyesho yake matano aliyoyafanywa huko Oslo.
Maonyesho hayo huvutia nadhari ya vyombo vya habari licha ya kwamba mwanzoni watu walikuwa wanasema yalikuwa yamezidi hali ya kawaida na kwamba yalikuwa hayakubaliki. Hivyo, Håvve alionyesha moja ya maonyesho yake akiwa amefunikwa mwili wake katika mabandeji yaliyopakwa udongo maalum mweupe uitwo “plaster”. Alifanya hivyo akiwa mbele ya jumba hilo la makumbusho kupinga jinsi kazi zake zilivyokuwa zinakaguliwa.
hapa akitoboa paji lake la uso.
No comments:
Post a Comment