Haya wadau kombe la dunia hiloo bado kama mwezi mmoja unavyo ona kweye picha. ni moja ya Basi kutoka kwa majirani zetu wa kenya likiwa limepambwa kwa ajili ya world cup litakalo kuwa likikata bunga kutoka Nairobi hadi hadi south Africa . haya wenye mabasi bongo habari ndio hiyo!!!
Wednesday, March 31, 2010
Jela Miezi Sita Kwa Kumuonyesha Kidole cha Kati Mwarabu
Raia wa Uingereza anayeishi Dubai huenda akatupwa jela miezi sita kwa kosa la kumtukana kwa kumuonyesha kidole cha kati mwanafunzi wa kiarabu toka Iraq.
Simon Andrews, raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 56 anakabiliwa na hukumu ya kwenda jela miezi sita iwapo atapatikana na hatia ya kumuonyesha kidole cha kati mwanafunzi wa urubani toka Iraq. Gazeti la The Sun la Uingereza limeripoti kuwa Simon alishindwa kuzizuia hasira zake wakati wa ugomvi wake na mwanafunzi Mahmud Rasheed na kuamua kumtukana kwa kumuonyesha kidole cha kati. Mahmud alikimbilia polisi kupeleka malalamiko yake na haikuchukua muda mrefu Simon alitiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka mahakamani. Simon amepigwa marufuku kusafiri nje ya Dubai tangia alipotiwa mbaroni mwezi wa nane mwaka jana. Akitoa ushahidi wake mahakamani siku ya jumapili, Simon alijitetea kuwa hakufanya kitendo hicho na kwamba raia huyo wa Iraq anamsingizia. Mahmud hakujitokeza mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya Simon na pia hakuna mtu aliyejitokeza kama shahidi wa kesi hiyo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi aprili nne wakati uchunguzi zaidi ukiendelea. | ||
|
Monday, March 29, 2010
WAZIRI AFUNGA NDOA YA KISHOGA
Chris Bryant (kushoto) na Jared Cranney baada ya kufunga ndoa yao ya kishoga katika Viwanja vya Bunge la Westminster.
Ndoa hiyo ilikuwa ya kwanza kufanyika katika viwanja vya jengo hilo la Bunge baada ya Spika John Bercow kupata leseni husika kutoka Halmashauri ya Jiji ya Westminster.
Katika taarifa iliyotolewa baadaye, wanandoa hao walisema walikuwa na “furaha kubwa” kwa Bw. Bercow na kiongozi wa Bunge la Makabwela, Harriet Harman kwa “kufanikisha siku hiyo maalum”.
"Hatukufikri siku hii ingefika, hatukuhangaika kuhusu keki, maua na pete,” walisema na kuongeza: “Ni ajabu hivi sasa mambo yamebadilika katika muda mfupi. Zamani mashoga walikuwa hawawezi kuoana bila kufikia umri fulani, walikuwa wanabaguliwa mpaka jeshini, hawakuruhusiwa kuoana au kupewa watoto wa kuasili.”
Walilisifia bunge kwa kufanikisha jambo hilo na kwamba kila mtu nchini Uingereza angepata fursa hiyo ambayo ilikuwa adimu.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, mwaka jana aliruhusu madai ya watu wa jinsia moja kuoana.
Hivyo ndoa zinaweza kufanyika katika viwanja vya Bunge, lakini si katika kanisa la sehemu hiyo ambalo halikubaliani na ndoa za watu wa jinsia moja.

Mtoto wa China Mwenye Vidole 31
Mtoto huyu wa nchini hana idadi ya vidole vya miguu na mikono kama watu wengine, amechukua rekodi ya dunia kwa kuwa na jumla ya vidole 31
Mtoto mwenye umri wa miaka sita wa nchini China analazimika kufanyiwa operesheni ili kupunguza idadi ya vidole vyake vya mikono na miguu.
Mtoto huyo wa mji wa Shenyang katika jimbo la Liaoning kaskazini mwa China ana jumla ya vidole 16 vya miguu na vidole 15 vya mikono.
Vidole vyake vitatu katika kila mkono wake vimeungana pamoja.
Idadi ya vidole vyake inavunja rekodi ya dunia ya vidole 25 iliyokuwa ikishikiliwa na watoto wawili wa India Pranamya Menaria na Devendra Harne, ambao kila mmoja wao ana vidole 12 vya mikono na vidole 13 vya miguu.
Hata hivyo mtoto huyo wa nchini China atafanyiwa operesheni ya kupunguza idadi ya vidole vyake wiki hii.

Wednesday, March 17, 2010
Mtu wa Kwanza Duniani Ambaye Hana Jinsia
Mlowezi wa kiingereza nchini Australia ameingia kwenye rekodi za dunia kwa kuwa mtu wa kwanza kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote si ya kiume wala ya kike.
Norrie May-Welby mwenye umri wa miaka 48, Muingereza anayeishi nchini Australia amekuwa mtu wa kwanza duniani kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote.
Madaktari nchini Australia walishindwa kumuweka Norrie kwenye fungu la wanawake au wanaume kutokana na hali yake ya kutokuwa na viungo vyovyote vya siri.
Norrie alizawaliwa kama mwanaume lakini alifanya operesheni ya kubadilisha jinsia yake kuwa mwanamke mwaka 1990 wakati huo akiwa na umri wa miaka 28.
Lakini baada ya kutokuwa na furaha katika hali yake mpya ya uanamke, Norrie aliamua kufanya operesheni nyingine na kuondoa uke alioupandikiza ili asiwe na jinsia yoyote.
Katika pasipoti yake mpya kama raia wa Australia, ilibidi maafisa wa serikali waongeze fungu jingine la watu wasio na jinsia baada ya madaktari kusema kuwa wanashindwa kuthibitisha Norrie ni jinsia gani.
"Mimi si mwanaume wala mwanamke, mimi nimeona bora nisiwe na jinsia yoyote", alisema Norrie.
Kutokana na uamuzi huo wa maafisa wa Australia, Norrie amekuwa mtu wa kwanza duniani kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote.

Tuesday, March 16, 2010
JAMAA ASIYESIKIA MAUMIVU!
Håvve Fjell, Mtu asiyesikia maumivu akiwa katika kazi zake.Håvve Fjell hujaribu kuonyesha kwamba huwa hasikii maumivu. Maonyesho anayoyafanya jamaa huyo wa Norway, hakika yanapagawisha kiasi cha kuonekana kwamba si jambo la kweli kwa mtu mwenye hisia za asili...
Baada ya kuanzisha sanaa hiyo aliyoiita “Pain Solution” mwaka 1993, Fjell alipata fursa ya kushirikiana na watu wengi walioipenda, na leo hii watu wengi zaidi hupenda kusoma kitabu chake kiitwacho "Kvintett," ambacho kinaonyesha mfululizo wa maonyesho yake matano aliyoyafanywa huko Oslo.
Maonyesho hayo huvutia nadhari ya vyombo vya habari licha ya kwamba mwanzoni watu walikuwa wanasema yalikuwa yamezidi hali ya kawaida na kwamba yalikuwa hayakubaliki. Hivyo, Håvve alionyesha moja ya maonyesho yake akiwa amefunikwa mwili wake katika mabandeji yaliyopakwa udongo maalum mweupe uitwo “plaster”. Alifanya hivyo akiwa mbele ya jumba hilo la makumbusho kupinga jinsi kazi zake zilivyokuwa zinakaguliwa.
hapa akitoboa paji lake la uso.
Mwanaume Mfupi Kuliko Wote Duniani Afariki Dunia
He Pingping, amefariki dunia nchini Italia akiwa na umri wa miaka 21.
He alikuwa nchini Italia kwaajili ya kushiriki katika shoo moja ya luninga iitwayo "The Record Show" lakini alisumbuliwa na maumivu makali kwenye kifua na aliwahishwa hospitali ambapo alifariki siku ya jumamosi kutokana na kile kinachoaminika kuwa ni matatizo ya moyo.
Monday, March 15, 2010
JOHAN LORBEER MJERUMANI ANAEGANDA UKUTANI.
Cheki maajabu haya, jamaa Johan Lorbeer wa huko nchini Ujerumani, akionyesha ujuzi wake wa kuganda ukutani, na watu wanashangaa sana haya maajabu, anawezaje kuganda ukutani bila kushikilia?, hakuna waya wala kitu chochote kinacho mshikilia (unachoweza kukiona)....ila kutakuwa kuna mbinu fulani imetumika, sasa sijui ndo mazingaombwe yenyewe haya?
Tuesday, March 9, 2010
Bibi wa China Aota Mapembe Kama Mbuzi
Bibi mwenye umri wa miaka 101 wa nchini China anawashangaza mamia ya watu kutokana na mapembe kama ya mbuzi yanayoendelea kujitokeza kwenye kichwa chake.
Bibi Zhang Ruifang mwenye umri wa miaka 101 wa kijiji cha Linlou katika jimbo la Henan nchini China alianza kuota pembe moja kwenye kichwa chake mwaka jana. Hadi sasa pembe hilo lililoota kwenye upande wa kushoto wa paji lake la uso limekua na kufikia urefu wa sentimeta sita. Upande wa kulia wa paji lake la uso kuna pembe jingine ambalo ndio kwanza linaanza kujitokeza. Familia yake imepagawa na mapembe hayo na haijui kwanini yanajitokeza kwenye kichwa chake. Mtoto wa mwisho wa bibi huyo anayeitwa Zhang Guozheng mwenye umri wa miaka 60 alisema kuwa wakati mapembe hayo yalipoanza kujitokeza mwaka jana hawakujali sana walidhania ni makunjamano ya ngozi tu. "Lakini siku zilivyozidi kwenda pembe lilijitokeza kwenye kichwa chake na sasa limefikia sentimita sita" alisema Zhang ambaye kaka yao wa kwanza ana umri wa miaka 82. "Hivi sasa kuna kitu kinajitokeza kwenye upande wa kulia wa paji lake la uso bila shaka ni pembe jingine", aliendelea kusema Zhang. Madaktari walisema kuwa mapembe hayo yanaweza kuondolewa kwa operesheni lakini sababu ya kujitokeza kwa mapembe hayo bado haijulikani. | ||
Monday, March 8, 2010
Thursday, March 4, 2010
Kondomu Ndogo Kwaajili ya Watoto Zaingia Madukani
Kondomu zenye ukubwa wa wastani zinadaiwa kuwa haziwatoshi ipasavyo vijana wenye umri mdogo
Kampuni kubwa ya kutengeneza kondomu ya Uswizi imetengeneza kondomu ndogo sana kwaajili ya watoto kuanzia umri wa miaka 12 kutokana na kile kinachosemwa kuwa watoto wa siku hizi wanaanza kufanya ngono mapema.
Kondomu hizo zilizopewa jina la "Hotshot" ni maalumu kwa vijana wa kiume wenye umri mdogo kuanzia umri wa miaka 12 hadi miaka 14.
Kondomu hizo zilitengenezwa kufuatia hatua ya makundi ya uzazi wa mpango kusema kuwa vijana wenye umri mdogo hawapati kinga inayotakikana wakati wa kujamiiana.
Ilidaiwa kuwa vijana wa siku hizi wanaanza ngono mapema na hawatumii kinga na wala hawajui jinsi ya kujikinga na magonjwa yanayotokana na ufanyaji wa ngono zisizo salama.
Kondomu hizo zimeingia madukani nchini Uswizi na kuzua maoni tofauti toka kwa wazazi nchini Uswizi.
Taarifa ya utafiti uliofanyika kabla ya kutengenezwa kwa kondomu hizo ilionyesha kuhitajika kwa elimu ya mapema kwa vijana jinsi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa pamoja na mimba zisizohitajika.
Msemaji wa kampuni ya Lamprecht AG iliyotengeneza kondomu hizo, alisema kuwa watakapoanza kuuza kondomu hizo nje ya nchi, Uingereza itapewa nafasi kubwa kutokana na idadi kubwa ya mimba za wasichana wenye umri mdogo.
Katika nchi za ulaya Uingereza inaoongoza kwa idadi kubwa ya wasichana wanaopata ujauzito kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

Wednesday, March 3, 2010
Mtoto wa Miaka 2 Mwenye Kilo 41
Kwa umri ana miaka miwili tu lakini kutokana na unene wake mtoto huyu wa nchini China ana uzito wa kilo 41 na bado anaendelea kunenepa
Tuesday, March 2, 2010
Mambo ya Kili Marathon
Helkopta hii naambiwa ni ya raia wa Tanzania na imnunuliwa kwaajili ya Kmpeni za mwaka hu na zipo mbili. Hapa ilikodiwa kwaajili ya kurekodi picha za Mbio za Kilimanjaro Marathoni mjni Moshi.
Monday, March 1, 2010
NDEGE YAZUA KASHESHE MWANZA!
Habari kutoka Mwanza zinasema kuwa ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege Tanzania imepasuka matairi mawili ya mbele na kusababisha kizaaa kikubwa kwa abiria wapatao 36 na wafanyakazi 7 waliokuwamo ndani ya ndege hiyo, mapema leo asubuhi. Hali hiyo ilitokea wakati ndege hiyo ikijaribu kutua huku hali ya hewa ikiwa mbaya kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha karibu nchi nzima. Inaelezwa kuwa baada ya matariri ya mbele kupasuka, ndege ilitembelea tumbo kwa mita kadhaa kabla ya kufanikiwa kusimama na abiria pamoja na wafanyakazi wake kutoka salama. Safari za ndege kubwa zimesimamishwa kwa muda uwanjani hapo.
KILIMANJARO MARATHON 2010 YAFANA
Wakimbiaji wa mbio za kilomita 42 za Kilimanjaro Marathon 2010 wakianza mbio hizo zilizofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro jana.
Mzee huyu wa mika 67 kutoka mkoani Arusha, Ake Lingstone akimaliza mbio za kilomita 21 wakati wa Kukimbia Mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
Subscribe to:
Posts (Atom)