Thursday, December 31, 2009

Banana Investment LTD juu ya Kilimanjaro



Wadau wakiwa tayari kukwea mlima. hapa ni Machame gate

Mkurugenzi wa BIL Adolf Olomi (mwenye kofia nyekundu) akiwa na baadhi ya wafanyakazi...
safari inaendelea..


Hapa wadau wakiwa kituo cha Barafu...
ipo baridi si mchezo..


Hapo ndio wadau wamefika Uhuru Peak (kutoka kushoto) Emmanuel Nevava, Mathias, Adrian Anthony na Willy Kwayu. HONGERENI SANA WAZEE.

Mzee Kawawa afariki dunia


Habari za kusikitisha za asubuhi ya leo zinasema kuwa Mzee Rashid Mfaume Kawawa, ambaye alizushiwa kifo jana, amefariki dunia leo asubuhi hii. Taarifa fupi ya Radio One Stereo iliyotolewa muda mfupi uliopita, imethibitisha kifo hicho. Mzee Rashid Kawawa, anafariki leo ikiwa ni siku ya mwisho kabisa ya kumaliza mwaka 2009 na anakufa akiwa na umri wa miaka 83. Mzee kawawa, ambaye pia alikuwa akijulikana kwa jina la Simba wa Vita, ndiye aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Awamu ya Kwanza wa Serikali chini ya hayati Baba wa Taifa, JK. Nyerere. MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEPONI - AMIN!

Wadau wa Banana Investments Ltd waenda vikishen Serengeti


Wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza mvinyo safi wa ndizi walipata nafasi ya kwenda kula happy kwenye mbuga ya Serengeti

Mzee wa mnyama(mwenye kofia) nikiwa na mzee wa upepo ofisi kuu ya hifandi ya serengeti


Hapa mdau nikiwa na Mwalimu Nyerere, Mgunduzi wa mbuga ya Serengeti pamoja na wadau Michael (mwenye kofia nyeupe) na Shannel Ngolly Tumekula pozi na wazee wakubwa.


Mzee wa pori akiwa amekula mingo kando ya hippo pool anatega atakaye jichanaganya kunywa maji kichwakichwa halali yake.


Ebwanaae mambo ya shamba kubwa hayo vitoweo vya kumwaga lakin gusa uone. Huo ni msafara wa mbogo(Buffalo ) wanaenda kukata kiu hippo pool, je itakuwaje wakikutana na mzee wa pori?


huyu ni Twiga wa Serengeti akijipatia menu yake Acacia


Hapa nikiwa na wadau wengine kutoka kushoto John Thomas, Mzee wa mnyama, Christogen a. k.a Mzungu pamoja na Mzee Mwanga, mdau John alikuwa anasisistiza jambo hapo ni Seronera

Baada ya game drive mchana ilikuwa ni kula bata ndani ya dik dik camp site


Hawa washkaj sijui walikuwa wanaenda wapi..... huyu ni John na Fredy..


Lakini waliporudi hali ikawa hivi.. unaweza kuniambia walitumia nini? inaweza kuwa ni mambo ya mnyama nini?
kazi kwenu wadau.

Asubuhi unaamka upo imara, hapa nipo na mdau john baada ya sekeseke la usiku na fisi


Wakatu tunarudi kama kawaida tulipita Ngorongoro, na hapo nyuma yangu ni Crater

Wednesday, December 30, 2009

Karibuni ndani ya Hi Tanzania!

Ndugu zangu nimeamua kuanzisha blog hii ili kuwaleteeni mambo mbali mbali yanayojiri ndani na nje ya nchi yetu nzuri ya Tanzania. najua kuna vitu vingi ambavyo mtataka kujua kutoka kwangu na kwa wadau mbalimbali, mnakaribisha sana ndani ya blog yangu. Nahitaji michango ya mawazo yenu kwani najua hakuan binadamu ambaye amekamilika kila idara hivyo nawakaribisha wote mtakao penda kuchangia au kutoa maoni yenu.
Mdau wenu mzee wa mnyama Peter Mapunda

Simba wa Yuda mgonjwa kitandani Muhimbili

JK na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Rashid Mfaume Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jioni. Kulia ni profesa Victor Mwafongo. Mzee Kawawa alipelekwa hapo Muhimbili baada ya kujisikia vibaya na kupelekwa hapo kwa kuangaliwa. Vipimo vinaendelea kujua anasumbuliwa na nini na hali yake ni stable.

Maharamia wa Kisomali wakamata meli mbili zaidi

Maharamia wa Kisomali wameteka nyara meli mbili zaidi za mizigo katika ghuba ya Aden katika bahari ya Hindi siku ya Jumatatu. Kukamatwa huko kwa meli ya Uingereza ya St. James Park , na meli ya mizigo ya Panama , Navios Apollon , kuna maana wahalifu hao wa Kisomali hivi sasa wanashikilia kiasi ya meli 11 na karibu mabaharia 250...

Check adha wanayopata ndugu zetu wa Kilosa

Athari za mafuriko kilosa
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Morogoro, Ahamed Msangi ( kushoto) akiwaongoza baadhi ya askari na wananchi katika ujenzi wa mahema kwa ajili ya kuishi watu waliokubwa na mafuriko na nyumba zao kibomolewa na mafuriko hayo , kwenye shule ya Msingi Mazinyungu ya Mjini Kilosa. Picha zote na mdau John Nditi
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Magomeni , Mjini Kilosa wakipita kwenye barabara iliyojaa maji ya mafuriko ya mvua pamoja na mizingo mikononi na vichwani kwenda kwenye makambi yaliyotengwa mjini humo
Vijana wa mjini Kilosa akitumia fursa ya mafuriko yaliyowaathiri wakazi wa Kata mbalimbali za mjini humo kuwasafirishia mizingo yao kwa kutumia usafiri wa mkokoteni na kutoza gharama ya sh: 1,000 hadi 2,000 kutokana na umbali. Mama akimwesha uji mwanae mchanga baada ya kufikishwa eneo la kambi iliyotengwa kwa ajili ya walioathiriwa na mafuriko ya maji katika mji wa Kilosa kwenye Shule ya Msingi ya Kilosa Town. Mafuriko hayo yaliaza tangu Desemba 26, mwaka huu.
Baadhi ya wananchi waliokubwa na mafuriko ya mvua kutoka Kata ya Mbumi, wakitelemsha vifaa vyaao kutoka katika gari la Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mara baada ya kuwafikisha kambi ya Kilosa Klabu.
Kijana akikatisha katika barabara iliyojaa maji na baiskeli yake mgongoni
kambi ya dharura ya walioathirika na mafuriko kilosa
Mkazi wa Kilosa akielekea kwenye kambi ya dharura

MATUMIZI BOT YASHTUA SERIKALI

Habari zaidi zinasema BoT imesitisha nyongeza ya mikopo ya nyumba ya asilimia 50 iliyoidhinisha kwa wafanyakazi wake, hatua ambayo imekuja siku chache baada ya kuidhinishwa na menejimenti ya taasisi hiyo kubwa ya fedha.

Taarifa za matumizi hayo makubwa ya fedha hizo za walipakodi katika kujenga makazi ya gavana ziliripotiwa na Mwananchi Ijumaa iliyopita katika habari iliyoeleza jinsi nyumba ya kigogo huyo wa BoT ilivyogharimu Sh1.4 bilioni kuikarabati, kabla ya Ndulu kutoa ufafanuzi kuwa nyumba hiyo ilijengwa upya na si kwamba ilikarabatiwa.

Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano juzi, Mkulo alisema pamoja na kushtushwa na taarifa hizo, jambo hilo ni kubwa na linahitaji umuhimu wa kipekee kuchunguzwa ili walipakodi wajue ukweli wa matumizi ya fedha wanazoilipa serikali.
"Lazima tuchunguze ukweli wa taarifa hizo, maana hili ni jambo kubwa na linamhusu mtu mkubwa," alisema Mkulo katika mahojiano na gazeti hili.

Mkulo alisema kuwa alikuwa safarini nje ya nchi na kwamba baada ya kurejea nchini juzi, ofisi yake itatumia wiki hii kufanyia uchunguzi suala hilo na wiki ijayo atakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuweka mambo yote hadharani.
Akitoa ufafanuzi wa tuhuma hizo wiki iliyopita, licha ya kukiri matumizi hayo ya fedha, Profesa Ndulu alisema kuwa nyumba anayoishi ilianza kujengwa kutoka chini na kwenye kiwanja ambacho ni cha BoT.

"Nyumba haijakarabatiwa, imejengwa from the ground (kutoka chini)... ni tofauti kukarabati na kujenga nyumba mpya... huu ni upotoshaji wa wazi na kujaribu kuchafua mema," alilalamika gavana huyo.
Aliongeza: "Napenda taarifa sahihi ambazo hazipotoshi ukweli kwa maana taarifa kama hizo zinaharibu kila kitu, kizuri na kujenga taswira mbaya kwa wananchi, kitu ambacho si sahihi."

Mwananchi toleo la Desemba 23, mwaka huu iliripoti kuwa nyumba anayoishi sasa gavana huyo ilikarabatiwa kwa takriban Sh1.4 bilioni na kwamba ilikuwa kwenye mradi wa kukarabati nyumba za vigogo wanne wa BoT; ya Ndulu na manaibu wake watatu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nyumba nyingine ni pamoja na aliyokuwa akiishi gavana wa zamani, marehemu Daudi Balali ambayo Prof Ndulu alidaiwa kuikataa kwa kuwa haina bwawa la kuogolea.
Licha ya tuhuma hizo, BoT inalalamikiwa kwa kujiidhinishia mamilioni ya fedha za mikopo yenye tofauti kubwa ya viwango baina ya wafanyakazi wa chini na vigogo.

Katika hatua nyingine, BoT imesimamisha nyongeza ya mikopo ya nyumba kwa asilimia 50, ambayo menejimenti hiyo iliridhia nyongeza yake ambayo watumishi wa kada ya chini wangejipatia mkopo wa hadi Sh30milioni na vigogo hadi Sh100milioni.
Habari zilizolifikia Mwananchi na kuthibitishwa na Gavana wa BoT, Profesa Ndulu zimethibitisha kusimamishwa kwa mikopo hiyo.
Kabla ya kusimamishwa kwa mikopo hiyo baadhi ya watumishi wa taasisi hiyo walikaririwa na vyombo vya habari (siyo Mwananchi), wakilalamika kuwa nyongeza hiyo ililenga kuwanufaisha zaidi vigogo.

Walidai kuwa matarajio yao yalikuwa wafanyakazi wa kawaida wangepewa kipaumbele zaidi, lakini hali ikawa kinyume.
Kusimamishwa kwa mikopo hiyo pia kumeibua mitazamo tofauti kwa wafanyakazi wa taasisi hiyo, wengi wakionyesha mashaka kwa hatua hiyo wakidai inawaaminisha kuwa nyongeza hiyo ilikuwa na lengo la kuwanufaisha zaidi wakubwa.
"Hii inaleta mashaka kwani kama hapakuwa na tatizo ni kwa nini baada tu ya kuripotiwa kwenye vyombo vya habari ndipo ikasimamishwa?" alihoji mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo.

"Sina hakika sana juu ya sababu zilizofanya mikopo hiyo isimamishwe na hatua au marekebisho yanayokusudiwa kuchukuliwa, lakini hii inaweza kutoa picha kuwa kuna mambo hayakuwa sawa ndio sababu imesimamishwa baada ya vyombo vya habari kuiripoti."
Lakini juzi, Gavana Ndulu alisema lengo la kusitisha mikopo hiyo ni kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi hao kuhusu mikopo hiyo.

Alisema imebainika kuwa wafanyakazi hao hawakuwa na elimu ya kutosha kuhusu vyongeza hiyo ya viwango vya mikopo na kwamba ndio maana walikaririwa na vyombo vya habari wakilalamika.
Ndulu alifafanua kuwa upo umuhimu wa elimu hiyo kwa wafanyakazi ili wasije wakabeba mzigo wasiouweza kwa kuwa mikopo hiyo ina masharti mengi kwa mkopaji.

"Tumeongeza masharti mengi na hatutaki mtu abebe mzigo asiouweza. Tumegundua wafanyakazi wengi hawakuelewa na ndio maana tumeona kuna umuhimu wa kuelimishana kwanza," alisema Prof Ndulu.

"Pengine elimu ilipaswa itangulie kwanza. Mara nyingi hivi vitu ni kuelewana. Ilionekana wengi hawakuelewa ndio sababu wakalalamika kwenye vyombo vya habari. Kwa hali hiyo sasa tumeisimamisha mikopo hiyo kwanza na tayari nimewaagiza maofisa husika kusimamia utaoaji wa elimu hiyo."

Gavana Ndulu alisema mfuko huo wa mikopo kwa nyumba umekuwepo kwa muda mrefu na kwamba kilichofanyika ni kuongeza tu viwango vya mikopo ili kuendana na mabadiliko ya hali ya maisha.
Kuhusu chanzo cha pesa hizo, alisema si za serikalini bali zinatokana na operesheni mbalimbali za benki hiyo ikiwa ni pamoja na riba inayotokana na mikopo mbalimbali wanayoitoa kwa serikali na kwa mabenki mengine nchini.

Kuhusu masharti ya mikopo hiyo alisema inapotokea mtumishi amestaafu kabla ya kumaliza kurejesha mkopo huo, basi sehemu ya mafao yake hutumika kufidia kiasi kilichosalia.
BoT imekuwa ikiangaliwa kwa karibu tangu kuibuka kwa kashfa ya wizi wa zaidi ya Sh133 bilioni kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Taasisi hiyo pia imekumbwa na kashfa nyingine kama za bima ya maghorofa yaliyo jijini Dar es salaam na Zanzibar, kuongeza gharama katika uchapishaji wa noti na matumizi mabaya ya madaraka katika ujenzi wa maghorofa pacha.
Wafanyakazi wa benki hiyo pia wamejikuta kwenye kashfa za kufanikisha njama za wizi, kuajiriwa kwa kutumia vyeti vya kughushi na tuhuma za watoto wa vigogo kupewa ajira za upendeleo.

CHANZO: MWANANCHI

Mafuriko barabara kuu Arusha - Moshi

mafuriko barabara kuu ya moshi-arusha
Juu na chini ni gari aina ya fuso iliyokua inatokea Arusha kuelekea moshi ikiwa imeangushwa na mafuriko yaliyokuwa yamekatiza barabarani kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zinanyesha mkoani Kilimanjaro fuso hiyo ilianguka katika mbele kidogo ya kijiji cha kwa Sadala wilayani Hai mkoani kilimanjaro. Mafuriko hayo yalizuia magari kupita kwa muda wa lisaa na nusu.(picha na Woinde Shizza)
Fuso likiwa limelala ubavu
maji yaendayo kasi yakikatisha barabara

Tuesday, December 29, 2009

Hi Tanzania!

Karibuni ndani ya blog hii mjionee mambo mbalimbali