Eti hii ni adhabu kwa watoto wa shule fulani huko bara Hindi, lakini huu ni Ufedhulu ambao hautakiwi kufumbiwa macho hata kidogo, wapi wanahaki za kibinaadamu?
Thursday, April 29, 2010
Wednesday, April 14, 2010
Monday, April 12, 2010
Tuesday, April 6, 2010
Wajue Virusi,Minyoo na Trojan
Kosa ambalo watu wengi tumekuwa tukilifanya kwenye ulimwengu wa kompyuta ni kuweka kirusi,trojan na mnyoo kwenye kundi moja na yoote kuvipa jina moja la virusi,kila mara utasikia kompyuta yangu ipo taratibu mno,nadhani nimeingiliwa na kirusi,Haya maneno hutumika kumaanisha maana moja lakini tukirudi kweye tekinolojia ya computer,si kweli.Hivyo basi kwa kujua utofauti wake hii itakusaidia kuilinda kompyuta yako na uharibifu unaoweza kufanywa na virusi,trojan au monyoo
Kirusi ni nini?
Kirusi hujiweka chenyewe kwenye program au faili na kuweza kusafiri toka kompyuta moja hadi nyingine,kumbuka kuwa kipindi kinasafiri huacha madhara kwenye kompyuta husika,kama kilivyo kirusi kwenye mwili wa binadamu,kirusi cha kompyuta pia huweza kuleta madhara makubwa kuanzia kwenye software,mafaili hadi hardware.Kumbuka kuwa virusi vingi vinakuwa kwenye mtindo wa exucutable faili,hii inamaanisha hakiwezi kukuletea madhara hadi pale utakapo kiamsha kwa kurun,kama mwili wa binadamu tunaposema HIV and AIDS,kirusi cha kompyuta hakiwezi kusafiri chenyewe bila ya mkono wa binadamu kwa mfano kudownload software toka vyanzo visivyoaminika na ndani yake wameweka visuri,huku wakivipamba kwa majina mazuuuri eg key generator nk.
Watu wamekuwa wakiendelea kusambaza virusi kwa njia nyingi kama kutumiana email huku ikiwa na attachment ambayo ni faili la kirusi,bila kujua unalidownload na kuliweka kwenye kompyuta yako,pale utpolifungua tu unaona kompyuta yako imekuwa blue na kuanza kutoa maneno ya ajabuajabu,hicho ndio kirusi
Mnyoo
Mnyoo hufanana na kirusi kwa njia moja au nyingine,mnyoo huweza kusafiri toka computer moja hadi nyingine lakini huwa na tofauti na kirusi kidogo,mnyoo yeye huweza kusafiri bila ya msaada wa binadamu9(hauhitaji kuufungua ili kuweza kusafiri),mnyoo hutumia msaada wa kujificha ndani ya mafaili kuweza kusafiri toka computer moja hadi nyingine. Mnyoo ni mbaya zaidi ya kirusi kwa sababu yeye ana uwezo wa kujitengeneza ama kujimegamega ndani ya system yako,
Kwa mfano labda wewe ulipokea mnyoo mmoja baada ya kutembelea website X,hivyo bila wewe mwenyewe kujua niini kinaendelea huyo mnyoo huweza kujimega au kuzaana ,baada ya siku moja ndani ya kompyuta yak kuna minyoo kama elfu moja hivyo inaanza kujituma kwenda kwenye mail list yako nk,kumbuka sasa inakwenda minyoo miamia na mmojammoja.(Ni mara ngapi umekuwa uipokea e mail toka kwa mtu kwenye mail list yako iklist sijui nimeona hii web nzuri hivyo nawe tembeleaikikupa anuani ya hiyo web?) Hiyo ndio kazi mojawapo ya minyoo
Minyoo huathiri ufanyajikazi wa kompyuta ama network yako,hii ni kwa sababu yao yenyewe hutumia memory au bandwidth nyingi kujisafirisha na kuacha data nyingine zikifa njaa(quieing),katika tekinolojia ya leo,minyoo huweza hata kumpa nafasi mtu aliyeitengeneza kuweza kuimiliki kompyuta yako remotely(Hivyo kuwa makini hapo)
Trojan Horse
Trojan horse ni kati ya mdudu mmoja ambaye ni mjanja na mtundu huku ikihitaji umakini kukabiliana naye,ndio maana wakamuita trojan horse! Trojana mara nyingi huwa ni software ambazo zinatoka kwenye vyanzo vinavyoaminika na kama mtumiaji ni ngumu kudhani kama kunaweza kuwa na matatizo ndani yake,baada ya kuistall kwenye kompyuta yako matatizo ndio huanza ila huwa yanatofautiana toka trojan mmoja hadi mwingine,maranyingi huweza kufanya vitu vya ajabu ajabu kama kubadilisha picha kwenye desktop yako,kuweka icon za ajabuajabu nk,pia wanaweza kuanza kufanya mambo yenye madhara kwa kufuta baadhi ya mafaili,kuweka shortcut na mengineyo ambapo hapo sasa unaanza kuhisi umeingiliwa na kitu kwenye kompyuta yako.Vilevile trojan wana uwezo wa kumpa mtengenezaji uwezo wa kuiingilia na kuimiliki kompyuta yako remotely.
Trojana wanatofautiana kidogo na virus au minyoo kwani wao hawana uwezo wa kujitengeneza au kusumbua mafaili mengine
Suluhisho
Tumeelezea matatizo mengo sasa tuangalie njia ambazo unaweza kuzuia na kuifanya computer yako iwe salama
- Kumbuka kuiweka kompyuta yako up to date kwa kuinstall updates,uzoefu unaonesha kuwa mara nyingi watu wanaotumia OS za kuiba huwa waoga kuistall updates kwani wanaogopa labda microsoft atawawekea ile kitu inayoitaji validation,hehe.Unachotakiwa ni kutoichagua halafu unaendelea na kuistall updates nyingine.
- Tumia antivirus na kumbuka kudownload updates,kwani haya mashirika ya antivirus huwa yanatoa kinga pindi kirusi.mnyoo au trojan mpya anapoguundulika
- Hakikisha kuwa hiyo antivirus yako ina uwezo wa kuscan e mail na mafaili ambayo umeyanyonya toka kwenye internet
- Hakikisha unatumia firewall,huu ni kama ukutu wenye moto ambao huzuia program isiyohusika kuaccess kompyuta yako
- Jenga tabia ya kutotumia flash disk(USB) ambayo hutumika kwenye public kompyuta bila ya kuiscan
Subscribe to:
Posts (Atom)